Afisa habari wa Simba Haji Manara akimtambukisha kocha mpya Masoud Djuma (Kulia) aliyechukua nafasi ya Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya wa Simba Richard Robert leo katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.UONGOZI wa klabu ya Simba leo mchana umemtambulisha kocha mpya atakayevaa viatu vya aliyekuwa kocha msaidizi Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya anayechukua nafasi ya Dr Cosmas Kapinga.
Akitoa utambulisho huo mbele ya waandishi wa habari, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa Kocha Masoud Djuma kutoka Rayon Sports ya nchini Rwanda na kocha bora wa msimu uliopita kupitia klabu hiyo anakuja kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyeachia ngazi kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia nchini Uganda.
Manara amesema kuwa, kabla ya kufikia makubaliano ya kuachana na Mayanja tayari walikuwa wameshaanza mazungumzo na kocha Djuma kuja kusaidiana na kocha Jospeh Omog kuinoa klabu hiyo.
Akizungumza baada ya kutambulishwa Kocha Djuma, amesema kuwa amekuja Simba kusaidiana na kocha Omog kuwezesha kupata mataji mbalimbali na sio kufanya maajabu kama watu watakavyodhani.
“Sijaja kufanya maajabu, nimekuja kuisaidia Simba kwa kidogo nilichonacho ili kuisogeza mbele zaidi ”, alisema Djuma huku akiweka wazi zaidi kuwa amekuja kufanya kazi na falsafa yake ni kocha mwenye pande mbili mkali na mpole lakini huwa mkali pale ambapo mchezaji anataka kuharibu kazi.Kocha Masoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulisha na afisa wa habari wa Simba Haji Manara (Kulia) akichukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyejiuzulu jana.
“Mimi ni mtu wa pande mbili kwa ufupi ni kama kiganja cha mkono, kina pande mbili. upande mmoja mpole lakini kwa upande mwingine ni mkali. Nimekuja hapa kufanya kazi ili kuipeleka Simba mbele na mimi nisogee mbele.”amesema Djuma.
Kuelekea mechi ya watani wa jadi Okotoba 28, Djuma ameweka wazi kuwa toka amezaliwa ameanza kusikia Simba na Yanga kwahiyo anazijua vizuri , “Nimezaliwa nimekuwa nazisikia Simba na Yanga, kila sehemu kuna mechi zenye presha kubwa siwezi kuahidi lolote kuhusu mechi ya Simba na Yanga kwa sababu mpira una matokeo matatu.”
Ili kuliboresha benchi la ufundi, Klabu ya Simba imemtambulisha meneja anayerirhi mikoba ya Cosmas Kapinga, Richard Robert mwenye uzoefu wa masuala ya mpira na utawala ambapo awali aliwahi kuwa meneja wa wanja wa ndege na pia katika kituo cha JKM Park.
sábado, 21 de octubre de 2017
Kauli ya Rais Magufuli Kuhusu kufuta mbio za Mwenge
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa katika kipindi chake cha uongozi, Mwenge wa Uhuru utaendelea kukimbizwa nchi nzima kila mwaka, na kwamba hatakubali ufutwe kama ambavyo baadhi ya wanasiasa na wananchi wengine wamekuwa wakishinikiza.
Akizungumza akiwa Mkoa wa Mjini Magharibi mjini Zanzibar katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Miaka 18 ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana, Rais Magufuli amesema siyo yeye tu, kwani hata Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Shein watakaokubali kufutwa kwa mwenge huo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo mashinikzo kutoka kwa watu mbalimbali nchini wakitaka mwenge wa uhuru ufutwe kwa madai kuwa umekuwa ukiigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha katika kipindi chote cha miezi 6 ambacho huwa unakimbizwa nchi nzima.
Akiyasema hayo, Rais Magufuli alitoa sababu tatu, kwanini katika kipindi chake mwenge hautofutwa ambapo, moja ya sababu ni kuwa, mwenge huo unachochea maendeleo ya nchi.
Rais Magufuli amesema wale wanaosema kuwa mwenge unatumia fedha nyingi hawajui namna unavyoendeshwa kwani mwenge unapopita katika kila halmashauri, huwa wanahakikisha wanamradi mpya ambao utazinduliwa mwenge utakapofika, na hii huwalazimu kujituma zaidi katika kujenga miradi.
Lakini Rais alieleza kwamba, mwaka 2017 serikali ilitenga Tsh 460 milioni kwa ajili ya mbio za mwenge, lakini umezindua miradi ya mabilioni pamoja na kubaini miradi mingine ambayo ni mibovu na kuamuru wahusika kuchukuliwa hatua. Rais amesisitiza kwamba, kama mbio za mwenge zisingefanyika, huenda viongozi wa vijiji wasingejituma kufanikisha miradi hiyo, na hata hiyo mibovu isingebainika.
Sababu ya pili ya kutokufutwa kwa mwenge huo, Rais alisema kwamba unaunganisha watanzania. Akitolea ufafanuzi suala hili, Rais Magufuli amesema kwamba, kwanza mwenge hukimbizwa katika pande zote za muungano, lakini pia watu wanaoukimbiza hutoka pande zote.
Jambo hili ni muhimu sana kwa sababu linadumisha muungano wetu, kuimarisha ushirikiano pamoja na kudumisha
Subscribe Our Channel: https://goo.gl/pnWPWT.
Follow and Like Us On Facebook: https://goo.gl/GU6zXr.
SHOW MORE
CCM ZANZIBAR YAIFARIJI FAMILIA ILIYOPATA AJALI YA MOTO NA KUFARIKI WATU WANNE.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu wa familia iliyopata msiba huo katika k...