Kwenye Leo Tena ya Clouds FM leo August
2, 2017 Mtangazaji Geah Habib ameifikisha Hekaheka iliyotokea Mtoni
Kijichi DSM ambako nyumba ya Harusi iligeuka kilioni baada ya mwanamke
kuolewa na kufariki saa 11 baadaye.
Inaelezwa kuwa siku ya tukio Bwana Harusi aliwapigia simu ndugu wa mkewe kuwapa taarifa ya kuumwa ghafla mkewe ambapo alikuwa analalamika kuumwa tumbo na kumkimbiza Hospitali usiku huo ambako baadaye alifariki.
Pichani ni bibi harusi
Tukio hilo linatajwa kutokuwa la
kawaida baada ya ndoa kufungwa saa Kumi Alasiri na Bibi Harusi kufariki
saa Kumi na Moja Alfajiri huku ikidaiwa kuwa alikuwa na ujauzito wa
Miezi Sita.Inaelezwa kuwa siku ya tukio Bwana Harusi aliwapigia simu ndugu wa mkewe kuwapa taarifa ya kuumwa ghafla mkewe ambapo alikuwa analalamika kuumwa tumbo na kumkimbiza Hospitali usiku huo ambako baadaye alifariki.
0 comentarios:
Publicar un comentario