Home »
» Mradi wa Kuwezesha Umilikishaji Ardhi ( LTSP ) Wapokelewa na Wananchi Wilayani KILOMBERO
Kiongozi
wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga akitoa Mada kuhusu Ujenzi na
Ukarabati wa Masjala za Ardhi katika Kijiji cha Sululu Wilaya ya
Kilombero Mkoani Morogoro,Uhamasishaji huu unaendelea unafanywa pia
katika Vijiji Vingine unafanywa na Wizara ya Ardhi, kupitia Programu ya
Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LAND TENURE SUPPORT PROGRAME -
LTSP),Programu hii inafanya utekelezaji wake ndani ya Miaka mitatu
katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga, Mkoano Morogoro.
 |
Baadhi
Wananchi ambao ni Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Sululu
wakiangalia ramani ya masjala ya Ardhi, inayotakiwa kujengwa katika
kijiji hicho,kupitia Programu ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi,(LAND
TENURE SUPPORT PROGRAME - LTSP), mradi ambao upo chini ya Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. |
 |
Mmoja
wa Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Sululu Wilayani Kilombero,
akichangia Mada iliyowasilishwa na Kiongozi wa Urasimishaji ndugu
Swagile Msananga, iliyokuwa ikihamasisha Ujenzi wa Masjala ya
kijiji,ambapo pamoja na mambo mengine,itatumika kuhifadhi hatimiliki za
kimila (CCROs),ambazo zitatolewa baada ya Programu ya kupima Ardhi za
Vijiji katika wilaya za Mfano za Malinyi, Kilombero na Ulanga
kukamilika. |
 |
Kiongozi
wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga katika Meza Kuu akiwa pamoja na
watumishi wengine kutoka Wizara ya Ardhi pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji
cha Sululu ( kushoto) na Mtendaji Kata kushoto kwake,akiandika kitu
kwenye karatasi zake ili kuweka kumbukumbu sawa,wakati wa mkutano wa
kuhamasisha Ujenzi wa masjala ya Kijiji,kupitia Programu ya kuwezesha
umilikishaji Ardhi (LAND TENURE SUPPORT PROGRAME) - LTSP ),mradi ambao
upo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi. |
 |
Kiongozi
wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga ( watatu kushoto ) waliosimama
akiwa kwenye Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha
Sululu Wilayani Kilombero, Morogoro. |
 |
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Sululu, akifungua mkutano wa Kuhamasisha Ujenzi wa
Masjala za Ardhi Wilayani Kilombero, Kupitia Programu ya Kuwezesha
Umilikishaji Ardhi ( LAND TENURE SUPPORT PROGRAME - LTSP ) mradi ambao
unasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. |
 |
Kiongozi
wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga,kupitia Programu ya LTSP chini
ya Wizara ya Ardhi inayotekelezwa katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na
Ulanga Mkoani Morogoro, akitoa Semina elekezi Juu ya Mradi huo, wenye
lengo la kupima mipaka ya vijiji na kutoa hatimiliki pamoja na
kuhamasisha Ujenzi wa masjala za Ardhi kwenye Vijiji. |
 |
Sehemu
ya Umati wa Wananchi wa Kijiji cha Sululu Wilayani Kilombero
wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Kuongozi wa Urasimishaji ndugu
Swagile Msananga,kuhusu umuhimu wa ujenzi wa Masjala ya Kijiji,kupitia
Programu ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi(LANDA TENURE SUPPORT
PROGRAME),Mradi unaosimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi. |
 |
Kaimu
kamishna wa Ardhi nchini Bi Mary Makondo, akifafanua Jambo kwa
Waandishi wa habari wilayani Ulanga, kuhusu mradi wa Kuwezesha
Umilikishaji Ardhi katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga,
ikiwemo upimaji wa Mipaka ya Vijiji na Utoaji wa hatimiliki kwa Vijiji
37 vya Wilaya hizo. |
 |
Mratibu
wa Mradi wa Kuwezesha Umilikishaji Ardhi, ambao upo chini ya Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndugu Godfrey Machabe akizungumza
Jambo Mbele ya Kaimu Kamishna wa Ardhi, Bi Mary Makondo muda mfupi Baada
ya kumalizika kwa Kikao na Watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
mkoani Morogoro kuhusu utekelezwaji wa Mradi wa LTSP. Picha zote na Hannah Mwandoloma |
0 comentarios:
Publicar un comentario