miércoles, 25 de octubre de 2017

CCM ZANZIBAR YAIFARIJI FAMILIA ILIYOPATA AJALI YA MOTO NA KUFARIKI WATU WANNE.

1
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu wa familia iliyopata msiba huo katika kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.

2
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi  Akisalimiana na baadhi ya wananchi na viongozi mbali mbali walioudhuria katika msiba huo.
………………………………………………………………………….
Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM)Z anzibar kimetoa mkono wa pole kwa familia iliyopata ajali ya kuungua moto nyumba na kusababisha vifo vya watu wanne huko katika kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi wakati wa kuifariji familia hiyo amesema CCM Zanzibar imesikitishwa sana na tukio hilo kwani limegharimu maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia.
 Dk. Mabodi alisema kwa niaba ya Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  anatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo na kuwasihi waendelee kuwa  na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha msiba huo.
“ Kupoteza watu  Wanne katika familia moja  ni jambo zito linalotia huzuni lakini tuendelee kuwa wavumilivu kwani Allah amewapenda zaidi na sisi tuliobaki tuendelee kuwaombea  dua ili wapate makaazi mema na kusamehewa madhambi yao”, alitoa nasaha hizo kwa maskitiko makubwa Dk. Mabodi.”
Mapema Sheha wa Shehia ya Fumba, Mohamed Suleiman alifafanua kuwa nyumba hiyo ilianza kuwaka moto majira ya saa 6:15 usiku Oktoba 21 mwaka huu, ambapo wananchi mbali mbali walianza juhudi za kuzima moto huo na kushindwa kuokoa watu waliokuwa ndani kwani uliku ni mkubwa.
Suleiman alisema wakati juhudi za kuzima moto huo zikiendelea waliwasiliana na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar ambacho kilifika na kusaidiana na wananchi hao ambapo walizima moto huo na kukuta watu wanne tayari wamefariki dunia.
Akidhibitisha tukio tukio hiloalisema chanzo cha moto huo ni hitilafu za umeme zilizoanzia katika waya wa jokofu (Friji) lililokuwa likifanya kazi wakati wa usiku.
Kamanda Nassir aliwataja watu waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Bahati Ali Ameir (40), Sinawema Abdalla Ali, Hashim Abdalla Ali (6) na Latifa Mohamed Ali (8).
Alitoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuzima vifaa vya umeme wakati wa usiku ambavyo havina umuhimu wa kutumiwa wakati huo ili kuepuka majanga yanayoweza kuhatarisha maisha ya watu.

JOTO LA KARIAKOO DERBY OCTOBER 28 UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

NGAO+PIC

Milango ya saa 10:00 jioni jumamosi ya Octoba 28, 2017 wapinzani wa jadi nchini katika soka wanakwenda kukutana ndani ya uwanja wa Uhuru katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara . Hawa si wengine bali ni mnyama Simba SC na wana jangwani Yanga SC.


Mchezo huo ni namba tatu Afrika kwa umaarufu katika soka ukitanguliwa na vinara Al Ahly dhidi ya Zamaleki pale jijini Cairo nchini Misri al maarufu kama Caira Derby . Mtanange wa wababe wa ligi kuu nchini Afrika kusini katika viunga vya Soweto Orlando pirates na Kaizer chiefs wanashika namba mbili wakisimama na jina la Soweto derby.
Timu hizi zinakutana huku kila mmoja akiwa na ari, nguvu na hamasa kubwa ya kusaka ushindi ili kujitengenezea njia ya kulinyakua kombe la ligi kuu msimu huu pia kuweka heshima kwa mtani wake. Wote wana wana alama 15 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu lakini Simba SC akiongoza jahazi kutokana na wingi wa magoli . Hili peke yake linaleta mvuto wa aina yake kuelekea mchezo huo.
SIMBA SC
Kuelekea mchezo wa jumamosi, wanaonesha hamasa kubwa ya kuibuka wababe katika mtanange huo wa jadi . Upana wa kikosi chao , uwezo wa mchezaji mmoja mmoja , matokeo ya nyuma, uongozi katika ligi vitawafanya kusimama mbele ya Yanga wakiwa na mtaji mzuri wa kisaikolojia kuliko wapinzani wao na endapo wataitumia vyema fursa hiyo wanaweza kuibuka washindi jumamosi.
Msimu huu wa 2017-18 Simba wamefanya usajili mzuri tofauti na misimu kadhaa nyuma toka waliponyakua kombe la ligi kuu kwa mara ya mwisho mwaka 2012. Timu imekuwa na mseto mzuri wa vijana na wakongwe hali inayowafanya kuwa na kikosi kipana kuliko timu yoyote ndani ya ligi kuu kwa sasa . Upana wa kikosi chao ni uwezo unaoshabihana wa mchezaji mmoja mmoja katika kila eneo uwanjani hali inayolifanya benchi la ufundi la timu hiyo kuwa na nafasi kubwa ya kuipanga timu kulingana na mahitaji kwa mchezaji husika pia kutokuwa n hofu ya majeruhi au kuporomoka kwa kiwango cha mchezaji kuhatarisha ufanisi wao.
Mchezo wa mwisho wa Simba SC dhidi ya Mji Njombe walinzi wa kati walisimama Juuko Murshid na Jamali Mlipili aliesajiliwa msimu huu tokea Mbao FC . Akicheza mechi yake ya kwanza ndani ya jezi ya Simba, Mlipili alionesha uwezo mkubwa pembeni ya beki kisiki wa timu ya taifa ya Uganda nafasi ambayo mara nyingi husimama Method Mwanjali na Salimu Mbonde ambaye ni majeruhi. Hii ndio dhana ya upana wa kikosi .
Simba ina wachezaji ambao wana uwezo mkubwa kuamua matokeo ya mechi, kusimama vyema na mfumo na mbinu za mwalimu ili kuipa matokeo chanya timu hiyo endapo bahati ya ushindi itakuwa upande wao.
Ni dhahiri Aishi Manula golikipa namba moja wa timu hiyo na timu ya taifa atakaa langoni siku ya jumamosi Mungu akimjalia afya njema na utimamu wa mwili. Huyu ni golikipa bora wa ligi kuu nchini mara mbili mfululizo na tayari ana uzoefu wa joto la mechi hii akisimama imara langoni mechi ya ufunguzi wa ligi ya Ngao ya jamii dhidi ya Yanga . Manula alipangua penati Kelvin Yondani na kujipanga vyema langoni hali iliyomfanya Juma Mahadhi kujikuta anapaisha mkwaju wa penati na kuwapa ubingwa Simba SC hivyo anaiendea mechi hiyo akiwa vyema kisaikolojia dhidi ya Yanga pia anawajua vyema toka akiwa Azam FC akiwa sehemu ya kikosi kilichoipiga Yanga 4-0 katika mchezo wa Nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu.
Erasto Nyoni ni mchezaji mkongwe ndani ya ligi kuu Tanzania bara na huyu nina imani katika note book ya kocha mkuu wa Yanga SC George Lwandamina lazima yumo kuelekea mchezo huo adhimu kisoka nchini. Erasto ni kiraka eneo lote la ulinzi pia akiwa na uwezo mkubwa kucheza kama kiungo mkabaji. Sifa kubwa mchezaji huyu ni uwezo wa kudumu na kiwango chake ndani ya dakika 90 akicheza kwa kujituma , nguvu , akili ya mpira na kutimiza vyema majukumu yake uwanjani. Akipangwa kama mlinzi wa pembeni basi husimama imara kama mlinzi wa wing pia kiungo wa akiba wa pembeni kulinda n kushambulia. Uwezo wake huo ndio ulimfanya mechi ilyopita dhidi ya Njombe mji kuitengenezea magoli Simba kupitia wing ya kulia akicheza kama mlinzi wa kulia na kiungo wa pembeni. Ana uwezo mkubwa kuibana timu pinzani katika mashambulizi yake ya upande lakini pia akishirikiana vyema na wenzake kupandisha vyema timu . Endapo atapangwa jumamosi beki ya kulia , na benchi la ufundi la Yanga SC kumpanga Mwashiuya kama walivyofanya mechi ya juzi dhidi ya Stand United ni dhahiri kutakuwa na upinzani mkali . Kama Mwashiuya asipokuwa makini kwenye pressing atajikuta mipira mingi anaipoteza kabla ya kupiga krosi au kuukata uwanja . Mechi na Stand walikuwa wakifanya tactical overlapping na Ibrahim Ajibu pale ambapo Mwashiuya akipata mpira alikuwa akikokota kwa kuukata uwanja na Ajibu kutanua pembeni kitu ambacho Erasto ni mkongwe anaweza kuziba njia kwa kusogea juu kwenye edge ya 18 kuziba njia huku akifanya mawasiliano mazuri na walinzi wa kati kwa ajili aidha ya offside trick au covering.
Wengine ni Ally Shomari pia mlinzi wa kulia ambaye anaweza pia kuanza na kusimama vyema katika mechi hiyo , Zimbwe jr kushoto bado ni mwiba mkali katika ulinzi na kupandisha mashambulizi amecheza zaidi ya mechi tano za watani wa jadi hivyo hana pressure . Mkongwe Method Mwanjali kuna uwezekano mkubwa kuanza mechi hiyo akisimama na Juuko. Ana uwezo mzuri sema jazba na hasira za haraka ni kitu cha kuchunga kwake.
Safu ya kiungo ya Simba ndio eneo ambalo Yanga wanatakiwa kulipigia hesabu za mbali kidogo . Hapa ndipo patakapoamua matokeo ya jumamosi aidha sare , kufunga au kufungwa. Msimu uliopita Simba ilikuwa bora eneo la kiungo lakini wakawa butu kwenye safu ya ushambuliaji kwa sababu walikosa mtu wa kuiunganisha timu toka eneo la kiungo kwenda mbele .
Katika soka timu ikiwa bora kwenye ulinzi na kiungo ukaona inapwaya kwenye ushambuliaji kwa maana ya kushindwa kutumia nafasi wanazotengeneza ni dhahiri inamkosa namba 10 ( playmaker ) mwenye uwezo wa kuunganisha kazi za viungo wa kati na pembeni ( technical link up ) kumzunguka mshambuliaji wa kati au kuitanua vyema safu hiyo ili iwe na uwezo wa kutengeneza washambuliaji zaidi ya wawili inapoingia kwenye final third . Ujio wa Emanuel Okwi umetibu vyema tatizo la Simba SC katika hili ndio maana wana uwezo mkubwa wa kufunga . Okwi anasimama kama playmaker na mshambuliaji wa timu hiyo kitu ambacho kinawapa wakati mgumu wapinzani wake .
Si kwamba Omog anatengeneza mfumo wa ushambuliaji wa Simba kumzunguka mchezaji huyo , hapana kiufundi hili ni hatari na kwa uwezo wa kocha huyo sizani kama anaweza kufanya hivyo kwa maana anatambua akibanwa mchezaji huyo patterns zake zinakuwa zimefeli. Mechi na Mji Njombe alimpanga Mzamiru Yassin namba 8 kama kiungo wa juu akicheza sambamba na Jonasi Mkude huku Haruna Niyonzima akicheza wing ya kushoto na Okwi akicheza kama ‘ false 10’ . Kuna mbinu alikuwa anaijaribu Omog kuelekea mchezo wa jumamosi kupitia Njombe mji na kwa kiasi alifanikiwa . Aliwahadaa Mji Njombe kumchezesha Mzamiru kama kiungo mchezeshaji lakini alimpanga kama kiungo mshambuliaji kamili ( kifucho ) . Majukumu ya kuchezesha timu yalikuwa ya Niyonzima akibadili mifumo ya pasi uwanjani , kufunga na kufungua uwanja huku Okwi akitoka kucheza kama namba kumi na kucheza huru kulia na kushoto kwenye final third kama kiungo mshambuliaji namba mbili. 4-3-3 inahitaji viungo washambuliaji zaidi ya wawili. Endapo Yanga wataingia uwanjani kumtazama Okwi tu kwenye safu yao ya ulinzi watakuwa wamekosea na wanaweza kuumia . Umakini unahitajika kwa kuwatizama Simba wanapoanza kutoka nyuma kwenye wings na kati ni akina nani wanaenda timu kabla ya kuingia kwenye eneo lao la ulinzi.
Wapo wengi katika kiungo kwa upande wa Simba ; Ndemla huyu mara nyingi huanzia benchi kutokana na uwezo mkubwa wa kuwasoma wapinzani. Mara kadhaa amekuwa mwiba kwa Yanga kwa kutokea benchi na kubadili matokeo . Matokeo ya 3-3 msimu wa Brandts kwa Yanga huyu ndio alikuja kuikoa Simba wakiwa nyuma kwa goli tatu sambamba na Lucian. Kichuya kulia ni viungo James Kotei na pacha wake Jonasi Mkude ambaye amerudi vyema katika kiwango chake ni watu ambao wanaweza kuichachafya Yanga eneo la kati.
Kwenye ushambuliaji driving force kubwa ya Simba inaanzia kati na kwenye wings . Erasto Nyoni kulia na Zimbwe junior kushoto wana uwezo mkubwa kupanga mashambulizi sambamba na viungo wa pembeni Shiza Kichuya na Haruna Niyonzima ili kuwalisha vyema wachezaji wa kati Emanuel Okwi , Mavugo na Juma Luizio . Yanga kwa sasa si imara sana kwenye wings kama misimu miwili ya nyuma kutokana na kuondokewa na nyota wake kadhaa. Pengo la Saimoni Msuva kulia bado ni kubwa ambaye alikuwa akiwakaba wapinzani kwa kuwashambulia muda wote . Pius Buswita ana kazi ya ziada kuzima kazi ya Zimbwe na Niyonzima kwa jumamosi ili kuwanyima fursa kupitia kwenye wings.
Mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kuondoka kocha msaidizi Jakson Mayanja na ujio wa mburundi Masoud Djuma siyapi sana nafasi kuleta badiliko kubwa hususani kimbinu lakini yanaongeza hamasa ya upambanaji bado Simba itatembelea mipango na mbinu za Omog kuliko Masoud ambaye ni kocha msaidizi na bado hajapata muda wa kutosha na timu.
YANGA SC
Baada ya kuitazama Simba SC kiundani sasa tuwaangazie mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara ambao ndio watakuwa wenyeji wa mechi hiyo dhidi ya mahasimu wao Simba SC.
Kama ilivyo Simba, Yanga pia wanaingia katika mechi hii wakiwa na mtaji mzuri kisaikolojia , kimbinu , kiufundi, ari ya kupambana na hamasa kubwa ya kulinda heshima yao ya soka nchini kama mabingwa mara tatu mfululizo pia wakitaka uongozi wa ligi baada ya kulingana pointi sawa na Simba lakini Simba wakiongoza ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga .
LWANDAMINA
Huyu ndio kocha mkuu wa Yanga ambaye anaingia kwenye mtanange huu akiwa na pressure kubwa kushinda mechi ya derby baada ya kucheza mechi tatu na kuambulia patupu baada ya kufungwa mechi tatu. Lwandamina msimu wa 2016-17 alianza na kupoteza 2-1 na Simba SC. Kwenye michuano ya Mapinduzi alifungwa na Simba kwenye mikwaju ya penati hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. Lwandamina na vijana wake katika mechi ya ufunguzi ligi kuu msimu wa 2017-18 al maarufu kama Ngao ya jamii alipoteza pia kwa mikwaju ya penati hali inayomfanya kabla ya mechi ya jumamosi kuwa na rekodi ya kufungwa mechi tatu na Simba SC na kuambulia sare moja!.
Rekodi hiyo inamfanya George Lwandamina kuingia kwenye Kariakoo Derby akiwa na pressure kubwa kuhitaji matokeo chanya ili kuwaaminisha wapenzi na wanachama wa timu hiyo uwezo wake wa kucheza mechi za Derby kama alivyokuwa Zambia na kikosi cha Zesco United. Umakini , uwezo wa kuisoma Simba , kuandaa vyema kikosi chake ni vitu pekee ambavyo vinaweza kumfanya kushinda mchezo huo na kujipa thamani mpya mbele ya wanachama . Raha ya ubingwa kwa timu hizi mbili ni mmoja kumfunga mwenzake .
Kifalsafa Lwandamina ni muumini mzuri wa soka la kushambulia linalochezwa kwa pasi fupi fupi zenye kasi zikihama kutoka box moja kwenda jingine kwa njia ya kati ambayo inawatumia walinzi wa kati , viungo wa kati na mshambuliaji kiongozi nyuma ya playmaker wa juu anaetengeneza daraja kati ya viungo na mshambuliaji wa kati. Aliwapumzisha Kelvin Yondani na Juma Abdul mchezo wa juzi dhidi ya Stand United kutokana nakuwa na kadi mbili za njano. Kama wangepata kadi kwenye mechi ile ni dhahiri mchezo wa jumamosi wangeukosa ! . Lwandamina humtumia Yondani kama mlinzi kiongozi wa kati ambaye ana uwezo wa kukaba na kushirikiana vyema na kiungo wa chini kuanzisha mashambulizi aidha kupiga mipira mirefu kwenye wings ( fast break / outer ) au give and go passes kuwatafutia mwendo viungo wa kati . Yondani anaetengeneza kombinesheni nzuri na sweeper Vincent Andrew pia ana uwezo wa kuwapanga vyema walinzi wa pembeni aidha kwenye mtego wa kuotea au kufanya marking hususani kuziba njia kabla ya mpira kufika.
Lwandamina ambaye msimu uliopita akiwa na Juma Mwmbusi kama kocha wake msaidizi aliyempokea toka Hans van der Pluijm , aliendeleza falsafa ya kushambulia kupitia pembeni kupitia mawinga kama Saimoni Msuva ambaye hivi sasa ametimkia Al jadida ya Morocco pia Deusi Kaseke wing ya kushoto. Lakini msimu huu baada ya mabadiliko makubwa ya kikosi hicho kwa wachezaji wengi kuondoka na wapya wengi kuingia , Lwandamina amebadili mifumo na mbinu zake kulingana na aina ya wachezaji alionao . Ukiitazama Yanga hivi sasa si timu ambayo inategemea tena wings kutafuta magoli. Yanga inaweka soka chini ambalo linasonga mbele kwa kutandaza mpira chini kutoka box moja kwenda jingine. Katika mechi 5 za awali ligi kuu msimu huu timu ilionekana kukosa kasi , uchache wa kutengeneza nafasi za kufunga pia ubutu wa safu ya ushambuliaji kufunga. Mechi mbili za mwisho dhidi ya Kagera Sugar na Stand United, timu imekuwa na nguvu , kasi , uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za kufunga na kufunga huku mfumo ukiruhusu kila mchezaji kucheza kwa uhuru na kujituma. Katika mechi mbili za mwisho Lwandamina akitumia 4-3-3 amepata magoli 6 ! akiwachapa Kagera 2 na kushinda 4-0 dhidi ya Stand United.
Eneo la kiungo amelifungua kunyumbuka katika kujenga mashambulizi pia kuilinda timu katika kushambuliwa. Pappy Tshishimbi licha ya kusimama kama kiungo mkabaji lakini takribani mechi mbili anamtengeneza kama kiraka akiwa uwanjani . Anatibua mipango ya wapinzani kuanzia juu, hushuka chini kukaba lakini pia hutanua kiungo kujilinda kwenye wings ili kuwakataa wapinzani kupitia pembeni ‘ huru’ kushambulia. Mechi na Kagera alimpanga juu kama kiungo mchezeshaji lakini na majukumu mawili kuhakikisha kiungo cha wapinzani wao hakisogei , hakitulii kupanga timu , kumsaidia Makapu kwenye blocking pia kumzunguka Ajibu acheze huru kwenye final third kama ‘ screening ‘ kwenye attacking pattern ndio maana kuna wakati Tshishimbi alikuwa anafanya driving kwenye final third ili Chirwa na Ajibu wafunguke kitu ambacho kilikuwa kinawafanya Stand kurudi nyuma sana na kuvuka kwenye marking zone yao. Hili pia siku ya jumamosi inawezeka akicheza na Rafael Daudi au Kamsoko kama atakuwa amepona.
Piusi Buswita ni mtaji mwingine kwa Lwandamina kwenye wings , hachezi kama winga teleza Saimoni Msuva kwa maana ya ‘ sprinting ‘ . Buswita kulingana na mfumo wa Lwandamina kwa sasa unaotumia pasi fupi fupi ( box to box ) anachezeshwa kama kiungo mchezeshaji wa pembeni anaeukata uwanja anaposhambulia kwa maana ya kuongeza mashambulizi makali ya kati kuwazunguka Ajibu na Chirwa sasa hili huwalazimisha wapinzani hususani walinzi wa pembeni kusogea kati na kuziacha wazi flanks ambazo Ajibu au Chirwa hutanua pembeni kwa ajili ya counter . Simba wasipokuwa makini na mfumo huu kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kucheka na nyavu.
Driving force ya Ajibu ambaye kwa sasa anachezeshwa kama mshambuliaji mchezeshaji ( playmaker ) ina faida kubwa kwa Yanga kutengeneza set pieces au ku unlock muhimili wa ulinzi kutokana na uwezo mkubwa wa kukokota mpira pia kuuficha mpira. Licha ya uimara wa kiungo cha chini cha Simba SC lakini bado sio wazuri sana kukabia juu au kuvunja mipango ya wapinzani kabla haijafika kwenye attacking zone , endapo wakimruhusu Ajibu na back up ya viungo wa kati na pembeni kuwa huru kwenye eneo lao la ulinzi hakika Yanga inaweza kucheka na nyavu kwa kuutazama mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa waliopata shida kuwazuia kwenye eneo lao la mwisho.
Wing ya kulia ya Simba SC kama atapangwa Erasto Nyoni na Shiza Kichuya , Lwandamina kuna uwezekano mkubwa wing yake ya kushoto kuendelea kumwamini Gadiel Michael na Mwashiuya ambayo kwenye edge juu wanapata sapoti ya Ajibu kwenye attacking patterns huku kwenye marking Tshishimbi kama kiungo kiongozi kati hufika kutibua au kuziba njia . Erasto mzuri kupanda na kushuka hivyo ni lazima wing iwe technical weight kubwa kumlazimisha kubaki chini kitu ambacho Lwandamina anakiweza kwa kufanya swtiching za namba mara kwa mara kati ya Ajibu , Chirwa na Mwashiuya kwenye pressing .
Sina shaka na uwezo wa Youthe Rostand kwenye lango la Yanga . Ana uwezo mzuri kucheza krosi na kucheza one against one. Kikubwa lazima aongee na walinzi wake wa kati kuziba vyema njia ya kati ambayo kinara wa mabao ligi kuu Emanuel Okwi ni fundi wa kuitumia. Wakiweza kumzuia Haruna Niyonzima kuchezesha timu na kuficha mipira pia wakimziba Mzamiru au Ndemla kulingana na seletion ya Omog basi watamfanya Okwi acheze chini zaidi kama deep playmaker kitu ambacho kitawafanya Yondani na Dante kuwa huru kama wataanza katika pacha hiyo.

sábado, 21 de octubre de 2017

SAA 24 ZA KUJIUZULU KWA JACKSON MAYANJA, SIMBA YAMTAMBULISHA KOCHA MPYA MRUNDI

Afisa habari wa Simba Haji Manara akimtambukisha kocha mpya Masoud Djuma (Kulia) aliyechukua nafasi ya Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya wa Simba Richard Robert leo katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.UONGOZI wa klabu ya Simba leo mchana umemtambulisha kocha mpya atakayevaa viatu vya aliyekuwa kocha msaidizi Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya anayechukua nafasi ya Dr Cosmas Kapinga. Akitoa utambulisho huo mbele ya waandishi wa habari, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa Kocha Masoud Djuma kutoka Rayon Sports ya nchini Rwanda na kocha bora wa msimu uliopita kupitia klabu hiyo anakuja kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyeachia ngazi kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia nchini Uganda. Manara amesema kuwa, kabla ya kufikia makubaliano ya kuachana na Mayanja tayari walikuwa wameshaanza mazungumzo na kocha Djuma kuja kusaidiana na kocha Jospeh Omog kuinoa klabu hiyo. Akizungumza baada ya kutambulishwa Kocha Djuma, amesema kuwa amekuja Simba kusaidiana na kocha Omog kuwezesha kupata mataji mbalimbali na sio kufanya maajabu kama watu watakavyodhani. “Sijaja kufanya maajabu, nimekuja kuisaidia Simba kwa kidogo nilichonacho ili kuisogeza mbele zaidi ”, alisema Djuma huku akiweka wazi zaidi kuwa amekuja kufanya kazi na falsafa yake ni kocha mwenye pande mbili mkali na mpole lakini huwa mkali pale ambapo mchezaji anataka kuharibu kazi.Kocha Masoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulisha na afisa wa habari wa Simba Haji Manara (Kulia) akichukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyejiuzulu jana. “Mimi ni mtu wa pande mbili kwa ufupi ni kama kiganja cha mkono, kina pande mbili. upande mmoja mpole lakini kwa upande mwingine ni mkali. Nimekuja hapa kufanya kazi ili kuipeleka Simba mbele na mimi nisogee mbele.”amesema Djuma. Kuelekea mechi ya watani wa jadi Okotoba 28, Djuma ameweka wazi kuwa toka amezaliwa ameanza kusikia Simba na Yanga kwahiyo anazijua vizuri , “Nimezaliwa nimekuwa nazisikia Simba na Yanga, kila sehemu kuna mechi zenye presha kubwa siwezi kuahidi lolote kuhusu mechi ya Simba na Yanga kwa sababu mpira una matokeo matatu.” Ili kuliboresha benchi la ufundi, Klabu ya Simba imemtambulisha meneja anayerirhi mikoba ya Cosmas Kapinga, Richard Robert mwenye uzoefu wa masuala ya mpira na utawala ambapo awali aliwahi kuwa meneja wa wanja wa ndege na pia katika kituo cha JKM Park.

Kauli ya Rais Magufuli Kuhusu kufuta mbio za Mwenge

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa katika kipindi chake cha uongozi, Mwenge wa Uhuru utaendelea kukimbizwa nchi nzima kila mwaka, na kwamba hatakubali ufutwe kama ambavyo baadhi ya wanasiasa na wananchi wengine wamekuwa wakishinikiza. Akizungumza akiwa Mkoa wa Mjini Magharibi mjini Zanzibar katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Miaka 18 ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana, Rais Magufuli amesema siyo yeye tu, kwani hata Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Shein watakaokubali kufutwa kwa mwenge huo. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo mashinikzo kutoka kwa watu mbalimbali nchini wakitaka mwenge wa uhuru ufutwe kwa madai kuwa umekuwa ukiigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha katika kipindi chote cha miezi 6 ambacho huwa unakimbizwa nchi nzima. Akiyasema hayo, Rais Magufuli alitoa sababu tatu, kwanini katika kipindi chake mwenge hautofutwa ambapo, moja ya sababu ni kuwa, mwenge huo unachochea maendeleo ya nchi. Rais Magufuli amesema wale wanaosema kuwa mwenge unatumia fedha nyingi hawajui namna unavyoendeshwa kwani mwenge unapopita katika kila halmashauri, huwa wanahakikisha wanamradi mpya ambao utazinduliwa mwenge utakapofika, na hii huwalazimu kujituma zaidi katika kujenga miradi. Lakini Rais alieleza kwamba, mwaka 2017 serikali ilitenga Tsh 460 milioni kwa ajili ya mbio za mwenge, lakini umezindua miradi ya mabilioni pamoja na kubaini miradi mingine ambayo ni mibovu na kuamuru wahusika kuchukuliwa hatua. Rais amesisitiza kwamba, kama mbio za mwenge zisingefanyika, huenda viongozi wa vijiji wasingejituma kufanikisha miradi hiyo, na hata hiyo mibovu isingebainika. Sababu ya pili ya kutokufutwa kwa mwenge huo, Rais alisema kwamba unaunganisha watanzania. Akitolea ufafanuzi suala hili, Rais Magufuli amesema kwamba, kwanza mwenge hukimbizwa katika pande zote za muungano, lakini pia watu wanaoukimbiza hutoka pande zote. Jambo hili ni muhimu sana kwa sababu linadumisha muungano wetu, kuimarisha ushirikiano pamoja na kudumisha Subscribe Our Channel: https://goo.gl/pnWPWT. Follow and Like Us On Facebook: https://goo.gl/GU6zXr. SHOW MORE

lunes, 9 de octubre de 2017

Jela kwa kumshika mwanaume mwenzie kiuno

Mwanaume mmoja ajulikanaye kama Jamie Harron ambaye ni raia wa Scotland anakabiliwa na kifungo cha miaka 3 mjini Dubai baada ya kugusa kiuno cha mwanaume mwingine wakiwa bar.
Mwanaume huyo ambaye ana umri wa miaka 27, alikamatwa kwa kile kilichosemwa kuwa ameonesha tabia mbaya hadharani kwa kumshika mwanaume mwenzie kiuno jambo ambalo halikubaliki kabisa kwenye jamii hiyo.
Kwa mujibu wa Jamie akiwa kwenye bar iitwayo Rock Bottom alikuwa anajaribu kuzuia kumwaga kinywaji chake kwenye baa hiyo iliyokuwa imejaa watu, kwa kuweka mikono mbele na kujikuta akimgusa mwanaume huyo kimakosa kwenye kiuno ikiwa anaepuka kumgonga.

Mradi wa Kuwezesha Umilikishaji Ardhi ( LTSP ) Wapokelewa na Wananchi Wilayani KILOMBERO



Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga akitoa Mada kuhusu Ujenzi na Ukarabati wa Masjala za Ardhi katika Kijiji cha Sululu Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro,Uhamasishaji huu unaendelea unafanywa pia katika Vijiji Vingine unafanywa na Wizara ya Ardhi, kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LAND TENURE SUPPORT PROGRAME - LTSP),Programu hii inafanya utekelezaji wake ndani ya Miaka mitatu katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga, Mkoano Morogoro.
Baadhi Wananchi ambao ni Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Sululu wakiangalia ramani ya masjala ya Ardhi, inayotakiwa kujengwa katika kijiji hicho,kupitia Programu ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi,(LAND TENURE SUPPORT PROGRAME - LTSP), mradi ambao upo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mmoja wa Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Sululu Wilayani Kilombero, akichangia Mada iliyowasilishwa na Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga, iliyokuwa ikihamasisha Ujenzi wa Masjala ya kijiji,ambapo pamoja na mambo mengine,itatumika kuhifadhi hatimiliki za kimila (CCROs),ambazo zitatolewa baada ya Programu ya kupima Ardhi za Vijiji katika wilaya za Mfano za Malinyi, Kilombero na Ulanga kukamilika.
Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga katika Meza Kuu akiwa pamoja na watumishi wengine kutoka Wizara ya Ardhi pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Sululu ( kushoto) na Mtendaji Kata kushoto kwake,akiandika kitu kwenye karatasi zake ili kuweka kumbukumbu sawa,wakati wa mkutano wa kuhamasisha Ujenzi wa masjala ya Kijiji,kupitia Programu ya kuwezesha umilikishaji Ardhi (LAND TENURE SUPPORT PROGRAME) - LTSP ),mradi ambao upo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi.
Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga ( watatu kushoto ) waliosimama akiwa kwenye Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Sululu Wilayani Kilombero, Morogoro.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sululu, akifungua mkutano wa Kuhamasisha Ujenzi wa Masjala za Ardhi Wilayani Kilombero, Kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi ( LAND TENURE SUPPORT PROGRAME - LTSP ) mradi ambao unasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kiongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga,kupitia Programu ya LTSP chini ya Wizara ya Ardhi inayotekelezwa katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga Mkoani Morogoro, akitoa Semina elekezi Juu ya Mradi huo, wenye lengo la kupima mipaka ya vijiji na kutoa hatimiliki pamoja na kuhamasisha Ujenzi wa masjala za Ardhi kwenye Vijiji.
Sehemu ya Umati wa Wananchi wa Kijiji cha Sululu Wilayani Kilombero wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Kuongozi wa Urasimishaji ndugu Swagile Msananga,kuhusu umuhimu wa ujenzi wa Masjala ya Kijiji,kupitia Programu ya kuwezesha Umilikishaji Ardhi(LANDA TENURE SUPPORT PROGRAME),Mradi unaosimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kaimu kamishna wa Ardhi nchini Bi Mary Makondo, akifafanua Jambo kwa Waandishi wa habari wilayani Ulanga, kuhusu mradi wa Kuwezesha Umilikishaji Ardhi katika Wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga, ikiwemo upimaji wa Mipaka ya Vijiji na Utoaji wa hatimiliki kwa Vijiji 37 vya Wilaya hizo.
Mratibu wa Mradi wa Kuwezesha Umilikishaji Ardhi, ambao upo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndugu Godfrey Machabe akizungumza Jambo Mbele ya Kaimu Kamishna wa Ardhi, Bi Mary Makondo muda mfupi Baada ya kumalizika kwa Kikao na Watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kuhusu utekelezwaji wa Mradi wa LTSP.
Picha zote na Hannah Mwandoloma

PROF TIBAIJUKA! Kaeleza changamoto baada ya Rugemalira kuwa matatizoni



Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amebainisha namna wanavyokabiliwa na changamoto katika uendeshaji wa Shule ya Wasichana ya Kajumulo Alexander iliyopo Bukoba baada ya mmoja wa wafadhili wa shule hiyo James Rugemalira kuwa matatizoni.
Prof. Tibaijuka amesema hakuanzisha shule kibiashara badala yake alijitoa kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na kuwainua kielimu ndio maana anajitoa kwa kile alichonacho kuwasaidia watoto hao kwa kushirikiana na wafadhili wake huku akisema kuwa kwa sasa amebaki mwenyewe katika kuchangia baada ya mfadhili wake mkubwa James Rugemalira kushikiliwa na Polisi.

domingo, 8 de octubre de 2017

Tamko la ACT Wazalendo baada ya JPM kuteua Katibu mpya wa Bunge



Magufuli jana October 7, 2017 alifanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo zimeongezwa Wizara mbili kutoka 19 za awali hadi 21 huku pia idadi ya Naibu Mawaziri ikipanda kutoka 16 hadi 21 ambapo mbali na mabadiliko hayo ya Baraza hilo, Rais pia alifanya uteuzi wa Katibu wa Bunge.
Kutokana na uteuzi huo, kumekuwa na mitazamo na maoni mbalimbali kutoka kwa watu binafsi, wasomi na vyama vya siasa na miongoni mwao ni Chama cha ACT Wazalendo ambao baada ya uteuzi wa Katibu wa Bunge, kimetoa tamko kupitia kwa
Katibu, Itikadi, Mawasialiano na Uenezi, Ado Shaibu.

Jana, Oktoba 7, 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya teuzi mbalimbali ikiwemo uteuzi wa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
ACT Wazalendo tunasikitika kusema Kwamba kama ilivyo desturi, Rais ameamua kuyaweka pembeni matakwa ya Sheria yanayoongoza mchakato wa uteuzi wa Katibu wa Bunge na kuamua kujichagulia apendavyo.
Kutokana na unyeti wa nafasi ya Katibu wa Bunge, na kwa minajili ya kuweka ‘check and balance’ pamoja na kulinda uhuru wa Bunge, kwenye mchakato wa uteuzi wa nafasi husika, sheria imeweka utaratibu wa kufuatwa kwenye uteuzi wa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo basi, mbali na Rais kuwa na mamlaka ya kumteua Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anapaswa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria ya Utawala wa Bunge – The National Assembly (Admintration Act), 2015. Kwa mujibu wa Kifungu cha 7(3) cha Sheria hiyo, Rais atateua jina moja kutoka miongoni mwa majina matatu yaliyopendekezwa na Tume ya Huduma za Bunge.
Jambo hili sio la hiyari. Ni sharti la lazima la sheria ambalo Rais analazimika kulifuata. Ndio maana kifungu husika kinasema “The Commision shall recommend three names” (Tume ni LAZIMA ipendekeze majina matatu).
Wajumbe wa Tume ya Huduma za Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 12(2) cha Sheria ya Utawala wa Bunge ni wafuatao:
1. Ndg. Job Ndugai, Spika wa Bunge
2. Ndg. Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge
3. Ndugu Jenister Mhagama – Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Bunge
4. Ndg. Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni
5. Ndg. Magdalena Sakaya – Kamishna wa Bunge (CUF)
6. Ndg. Peter Msigwa – Kamishna wa Bunge (Chadema)
7. Ndg. Salim Hassan Abdullah Turky – (Kamishna wa Bunge – CCM)
8. Ndg. George Masaju
9. Ndg. Mary Chatanda (Kamishna wa Bunge – CCM)
10. Ndg. Kangi Lugola-(Kamishna wa Bunge-CCM)
11. Ndg. Mussa Hassan Zungu-(Kamishna wa Bunge-CCM)
Kwa taarifa tulizonazo, hakuna kikao chochote cha Tume ya Bunge kilichoketi na kupendekeza majina kwa Rais kwa ajili ya uteuzi wa Katibu wa Bunge. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wote wa Tume ya Huduma za Bunge waliohojiwa na vyombo vya habari wamethibitisha pia kutofanyika kwa kikao hicho.
Hitimisho:
1. ACT Wazalendo tunaona kuwa uteuzi huu si tu ni mwendelezo wa Rais kufanya maamuzi bila kuzingatia sheria za nchi bali ni ushahidi mwingine wa wazi wa kudharau mhimili wa Bunge.
2. Ni matumaini yetu kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano na watu wote wanaopenda uhuru na uimara wa Bunge watasimama imara kuupinga uteuzi huu ambao ni kinyume na sheria.
3. Kama Rais hatatengua uteuzi huu na kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria za nchi, ACT Wazalendo kitalifikisha suala hili Mahakamani ili kupata ufafanuzi wa mahakama.
4. Ni wakati muafaka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuishauri serikali kwenye masuala ya kisheria kuwajibika. ACT Wazalendo tunaamini suala hili na vitendo vingine vya huko nyuma vimetokea kwa sababu ya moja ya sababu mbili. Inawezekana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa woga au uzembe, hamshauri Rais ipasavyo au Rais hafuati ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika yote mawili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kama anataka kulinda heshima yake binafsi na ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hana budi KUJIUZULU.

RAISI ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI NA WACHACHE WANG'OKA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Mgufuli ametangaza baraza lake dogo jipya la mawaziri lenye wizara 18, huku akiwabakiza mawaziri wa zamani 7 na kuingiza sura mpya katika baraza hilo litakalokuwa na jumla ya mawaziri na manaibu waziri 34 tu.
Aidha, katika baraza hilo Rais Dk. Magufuli ameacha wazi nafasi za uwaziri katika wizara nne ambazo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Ujenzi pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambazo amesema bado hajapata watu wa kuwakabidhi majukumu ya uwaziri.
Dk. Magufuli amesema serikali yake imepunguza bazara la mawaziri ili mawaziri walioteuliwa wakafanye kazi, na kusisitiza hakutakuwa na semina elekezi ambapo ameagiza fedha zaidi ya shilingi bilioni 2 zilizotengwa kwa semina hiyo kuchukuliwa na kutumika katika shughuli nyingine.
Aidha, Dk. Magufuli akatuma salamu kwa mawaziri aliowateuwa katika baraza lake ambao wanapenda kufanya sherehe wajue wamepewa kazi ngumu na iwapo watafanya sherehe hizo wajiandae na kufanya sherehe pia wakati watakapotimuliwa kazi.
BARAZA LA MAWAZIRI
Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri - George Simbachawene na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri - Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri - Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri - William Ole Nasha
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani
Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri - Ashantu Kizachi
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.
Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.
Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri - Harrison Mwakyembe
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri - Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri - Dk. Hussein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri - Charles Kitwanga.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri - William Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Mabula
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage.
Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalim
Naibu Waziri – Dkt. Hamis Kigwangala
Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri - Nape Nnauye
Naibu Waziri - Anastasia Wambura.
Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu Waziri– Inj. Isack Kamwela

sábado, 7 de octubre de 2017

MSIBA HARUSINI: Bibi harusi kafariki saa 11 baada ya kuolewa kisa?

Kwenye Leo Tena ya Clouds FM leo August 2, 2017 Mtangazaji Geah Habib ameifikisha Hekaheka iliyotokea Mtoni Kijichi DSM ambako nyumba ya Harusi iligeuka kilioni baada ya mwanamke kuolewa na kufariki saa 11 baadaye.


 Pichani ni bibi harusi
Tukio hilo linatajwa kutokuwa la kawaida baada ya ndoa kufungwa saa Kumi Alasiri na Bibi Harusi kufariki saa Kumi na Moja Alfajiri huku ikidaiwa kuwa alikuwa na ujauzito wa Miezi Sita.
Inaelezwa kuwa siku ya tukio Bwana Harusi aliwapigia simu ndugu wa mkewe kuwapa taarifa ya kuumwa ghafla mkewe ambapo alikuwa analalamika kuumwa tumbo na kumkimbiza Hospitali usiku huo ambako baadaye alifariki.

CCM ZANZIBAR YAIFARIJI FAMILIA ILIYOPATA AJALI YA MOTO NA KUFARIKI WATU WANNE.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu wa familia iliyopata msiba huo katika k...